Tunatambua na kuamini kuwa itikadi na falsafa ya “Dhamira ni Dira” yaweza kumfikisha aliyedhamiria mahali anapotaka kufika.
Dhamira ni Dira
KWA KUWA, Sisi ni wasanii, tuna vipaji katika tasnia hii, tuna nia ya kuungana na kufikia malengo yetu ya kuwa wasanii mahiri na wa kuigwa; NA KWA KUWA, Kuna idadi kubwa ya watu ambao wana vipaji na wana ndoto nyingi za kujiendeleza katika tasnia hii ya sanaa za maigizo ila tu hawajaona mahali sahihi pa kuendeleza sanaa yao; HIVYO BASI, Tunatambua na kuamini kuwa itikadi na falsafa ya “Dhamira ni Dira” yaweza kumfikisha aliyedhamiria mahali anapotaka kufika.